Unaambiwa Mbunge wa CCM aliyejiuzulu afunguka Makubwa

Mbunge aliyejiuzulu afunguka TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema kuwa Jimbo la Konde visiwani Zanzibar lipo wazi na taratibu za kujaza nafasi hiyo zitatangazwa hivi karibuni. Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC Dk Wilson Mahera kupitia taarifa yake kwa umma jana. Dk Mahera alisema NEC ilipokea barua kutoka kwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ikitaarifa kuwa, Mbunge Mteule wa Jimbo la Konde, Sheha Mpemba Faki, alikitaarifu chama hicho kuwa hayupo tayari kuwawakilisha wananchi wa Jimbo la Konde kutokana na changamoto za kifamilia. Alisema kutokana na hilo, NEC inautaarifu umma kuwa jimbo hilo lipo wazi na taratibu za kujaza nafasi hiyo zitatangazwa. “Tume ifanya hivyo kwa kuwa ilikuwa bado haijamjulisha Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano kuhusu kukamilika kwa uchaguzi katika Jimbo la Konde na kuchaguliwa kwa Mbunge huyo Mteule. Pia Tume ilikuwa haijamtangaza kwenye Gazeti la Serikali kama ilivyoelekezwa katika Kifungu cha 81 (c) cha Sheria ya Taifa y...